Kyalo
banner
nkyalo.neocities.org
Kyalo
@nkyalo.neocities.org
38 followers 98 following 89 posts
AI imekuwa urembo wa kifashisti. Basi sina hata sababu ya kuitumia kwa masomo yangu, wacha hata sanaa yangu. 🏳️‍🌈 SW/EN Tovuti yangu: https://nkyalo.neocities.org/
Posts Media Videos Starter Packs
Pinned
Je, unaweza tambulisha niliporudia mara kwa mara? 😭
Nilikuwa nisalimishe kuchora jicho hilo la pili. Lakini niliweza kulichora mwishowe.

#فن
#art #sanaa #pencil #drawing #xmen
Reposted by Kyalo
Today is my 26th B'day ( ´ ꒳ ` ) Thank you for being here with me
Repost is the best gift for an artist
Ni juzi tu nilisikia kasheshe eti wanauza nyumba yao... Tena nikasikia kuhusu ndoa yao kuisha... Nilishangazwa sana, "Eh! Na huyu anajua haya yote aje?" Leo Spotify walinipendekezea wimbo huu na Lo!!!!!!!!!!!!!! Hii albamu!!!
😂
David!!!!!!!!! 👀
Nitauchapisha mchoro wangu kesho...
Jamani, msinicheke...
Hili ndilo lilikuwa rejeleo langu. 😶‍🌫️
Leo nilijaribu kumchora Hell Girl na ni bayana ya kwamba kuchora "anime" si rahisi. Nilianza vizuri lakini ilifika pahali nilipoamua yanatosha.
Nimegundua kuwa nina tatizo na kuchora nyuso.
Nimeangukia dhahabu leo.
Nimeamua nitamaliza kutizama video zote badala ya "ku-doomscroll".
There's no logic at all. The internet is just AI interacting with AI. And we have an internet where revenue is driven by engagements and ads.
So the billionaire class is basically saying that they don't need humans anymore. They'll generate profits without having to do much.
Je, unaweza tambulisha niliporudia mara kwa mara? 😭
Nilikuwa nisalimishe kuchora jicho hilo la pili. Lakini niliweza kulichora mwishowe.

#فن
#art #sanaa #pencil #drawing #xmen
Niliharibu tovuti yangu.
Kwa yule atakaye hisi kunitembelea huko, niwie radhi kwa muda kiasi tu. Nitaitengeneza haraka.
Nimekuwa nikirudi hapa kuangalia kama watu wameweza kuuona mchoro huu.
Nilifurahishwa sana na mchoro huu na nimeupenda sana mpaka ninataka tu watu wauone.
Ni sawa kama itanichukua muda kupata watu watakao furahia sanaa yangu.
Lakini sasa nina hamu nyingi ya watu kufurahia kazi yangu.
Niliuchora mchoro huu juzi. Na singeweza kuuchapisha mpaka sasa.
Na nimegundua ya kwamba nikiweka *filters*, mchoro wangu unaonekana vyema zaidi. Ni kama nilitumia hizo kalamu nzuri kuuchora.
#art #sanaa #فان #deadpool.
Sijawahi soma kurasa mingi hivyo hata na Voice Assistance. Nitaandika uhakiki wangu baadae.
Jana ndio siku nilikuwa nimesema lazima nimalize kusoma "The Yacoubian Building". Na ilikuwa imepita zaidi ya siku tano hivi nikiwa sijakiguza kile kitabu. Basi WiFi iliacha kufanya na nikaamua kusoma. Niliweza kumaliza kurasa mia moja arobaini na nne hivi na siku moja, kisha kitabu chenyewe.
Nimevutiwa ❤️
Mchoro wa kulia ndio wa leo. Nimeona nina shida kubwa ya kuchora miguu vyema. Ya leo imetokea vibaya kuliko ya jana. 😑
Ishafika saa kumi ya jioni na sijasoma masaa yangu mawili ya Calculus. Basi imenijia ya kwamba leo ni Jumapili na ningependa iwe siku ya mapumziko.... 😂
Lakini ningependa kupiga zoezi, kuchora, na kusoma kurasa 15 za "The Yacoubian Building". Hizo hazichukui muda mrefu.
Sasa ni kucheza michezo ya simu pekee yake. Sihisi vibaya kwani kuna michezo mzuri nilizozipenda kama Monument Valley 1 na 2.
Itakuwa miaka mpaka niweze kujinunulia kompyuta nzuri. Lakini ninaweza ngoja. Wacha nipambane na masomo kwanza nisianguke mitihani tena kwa sababu ya Fortnite. Hii ni baraka.
Kompyuta ya mkononi yangu ilirudishwa jana jioni na nilikuwa nina furaha eti ningeweza kucheza Fortnite tena baada ya muda. Kumbe lo!! Hata Epic Games Launcher yenyewe ina shida kuenda. Nami nikaamua nitaanza kucheza Fortnite tena ile siku nitakuwa na teknolojia sambamba. Hata siezi cheza Among Us 😭
Nimerudi!!!!
🥰🥰🥰